skills za kitaa

Tuesday, April 29, 2014

Jackline Wolper Ampiku Agness Masogange Kwa Pedeshee Wa Kihindi, Ni Yule Aliyetoa Milioni 40 Kwa Ajili Ya Kumchumbia Masogange

Msanii Wolper akiwa na Prence Kass maarufu kama Muhindi wa Masogange
Katika hali isiyokuwa ya kawaida Xdeejayz imenasa picha za msanii nyota wa filamu za Kibongo Jackline Wolper akiwa na mfanyabishara mmoja wa kihindi mwenye pesa ndefu aliyefahamika kwa jina la Prence Kass maarufu kama Muhindi wa Masogange.
Agness  Masogange ambae aliwahi kutolewa barua ya uchumba na Muhindi huyo mapema mwaka huu, hata hivyo haikufahamika mambo hayo yaliishia wapi.
Picha hizo zinazowaonesha wawili hao wakiwa kwenye moja ya viunga vya Club ya usiku iliyopo Oysterbay/ Masaki ambapo hata hivyo uhalisia wa picha hizo unamuonesha Wolper akiwa bwii kiasi cha kuubetua mdomo wake ambapo sio kawaida kwa mtu mwenye ufahamu na staa kama yeye kupiga picha zenye pozi baya kama hizi.
Msanii Wolper akiwa na Prence Kass maarufu kama Muhindi wa Masogange hapa nyota huyo akionekana akiwa amelewa uso unamajibu kwani hilo sio pozi la kawaida la mdomo kuubetua kiasi hicho.Inatoka kwa mdau.

No comments: