MSANII anaye fanya tasnia ya filamu
nchini Recho Haule amefunguka kuwa amekuwa akifanya mazoezi kwa sasa ili
kuimarisha mwili na si kwamba anapunguza uzito ili aolewe kama baadhi ya watu wanavyodai.
Nyota huyo mefunguka hivyo baada
ya kuibuka tetesi zilizotufikia katika
gazeti hili kutoka kwa baadhi ya wasanii wa tasnia hiyo ya filamu.
"Kwa sasa nafanya mazoezi kwaajili
ya kutunza hali ya afya yangu,nimekuwa
nikifanya mazoezi ilikuutunza
mwili wangu uwe katika hali ya afya
njema,"alisema Recho .
Recho ambaye ni mnene kiasili ,yupo mbioni kuja na ujio mpya wa filamu iitwayo Vanessa in Dillema akiwa amewashirikisha baadhi ya wasanii wakongwe kwenye tasnia ya filamu ikiwemo Haji adam'Baba Haji',), Jennifer Kyaka 'odama' .
No comments:
Post a Comment