Rapper Kanye West na
Kim Kardashian wamekuwa wasiri kuhusu mtoto wao kuanzia jinsia yake kabla
hajazaliwa lakini hata baada ya kuzaliwa wamekuwa na kigugumizi cha kuliweka
wazi jina la mtoto wao wa kike waliyempata June 15 mwaka
huu.
Japokuwa wameficha
jina la mtoto wao, cheti cha kuzaliwa cha mtoto huyo kimeongea…chanzo cha
kuaminika kimeuambia mtandao wa TMZ kuwa cheti hicho kimeonesha jina la kichanga
wao kuwa ni ‘North West’.
Well, wameamua
kutumia dira zaidi kupata jina la mtoto au labda ni kwa sababu baba nae anajina
la dira ‘West’ ambalo linatoka kwenye familia yake,marehemu mama yake aliitwa
Donda West.Tetesi za awali ziliwahi kulitaja jina hili, lakini baadae
ikasemekana wanaweza kutumia utaratibu wa familia ya Kardashians ambayo majina
yao lazima yaanze na herufi ‘K’.
Kwa mujibu wa US
Weekly, mtoto huyo tayari ameshapata jina la ki-digital yaani a.k.a na anaitwa
‘Nori’ kama ufupisho wa jina lake. Kwa upande mwingine, imesemekana kuwa Kanye
West hayuko tayari kufanya biashara kwa kuuza picha za mtoto wake kama
alivyowahi kufanya Angelina Jolie na Brad Pitt mwaka 2008 walipouza picha za
mtoto wao kwa kiasi cha dola million 14.
Lakini baba North
West hapendi kupigwapigwa picha na labda asiingependa mwanae pia aingie kwenye
lens za paparazzi, chanzo kimeoja kimesema inawezekana Kim Kardashian akaamua
kuzitoa bure picha za mtoto wao kwa kuwa ana hulka ya kupiga
picha.
Inasemekana Weezy
(36) mwenye mzuka wa ajabu wa kuandika na kutema mistari anaweza kuachia nyimbo
nne maalum kwa mwanae Nori..kama alivyofanya swaiba wake Jay-Z alipoachia Glory
kwa ajili ya Blue Ivy.
No comments:
Post a Comment