skills za kitaa

Tuesday, June 4, 2013

Cheki Uwoya anavyofunguka Kwenye mtandao

"Maisha yana mambo mengi na  kila mmoja anajaribu kufanya kile ambacho anaweza kukifanya na kwa uwezo wa Mungu akafanikiwa kukikamilisha na hatimaye kufikia malengo yake  aliyonayo katika nafsi yake.
Ninacho amini mimi ni kuwa  hakuna mtu ambaye amekuja  duniani kwa ajili ya matatizo  na  machungu tu hata kama  unapitia matatizo vipi ziko tu siku za neema  ambazo  mwenyezi mungu atazileta kwako na wewe kufurahia  maisha yako hapa  ulimwenguni
 
 
Binafsi Naishi Mbezi Beach na  haya  ndiyo maisha  niliyonayo  sasa  namshukuru mungu  mimi na familia yangu  pamoja na mwanagu  Krish tunaishi katika  mazingira ya kawaida yanayotuweka  katika furaha  kila  siku".
Moja kati ya vitu ambavyo napenda na  namshukuru mungu kuvipata ni magari, Toyota Kluger ni moja  kati ya  kadhaa ambayo yapo kwenye parking yangu hapa nyumbani.



 Pozi la utulivu Irene Uwoya duu.

Jeep ni aina  nyingine ya ride ambayo sometime  nafanya  mtoko nikiwa sambamba na marafiki zangu ambao tumekuwa pamoja  tangu na tangu katika  kutafuta  maisha  na  kujiweka  katika  mazingira  tofauti kila siku.
 
 Duuu , eeeeee huyu ni Uwopya wa ukweli . Aaaaaa.

No comments: