skills za kitaa

Monday, February 9, 2015

Fainal Kombe la Afrika 2015 Ivory Coast yapeta


Ivory Coast iliishinda Ghana kwa mikwaju ya penati 9-8
Ivory Coast iliishinda Ghana kwa mikwaju ya penati 9-8
Timu ya soka ya Ivory Coast imenyakuwa taji la Kombe la Afrika la mwaka 2015 kwa kuitandika timu ya Ghana kwa mikwaju ya penati mjini Bata, Equatorial Guinea.

Nahodha wa Ivory Coast akikabidhiwa kombe
Nahodha wa Ivory Coast akikabidhiwa kombe
Ivory Coast imeshinda kwa mikwaju 9 ya penati huku Ghana ikipata mikwaju 8.
Yaya Toure akishangilia baada ya kukabidhiwa taji lao
Yaya Toure akishangilia baada ya kukabidhiwa taji lao
Boubacar Barry, 35, ndiye aliyeibuka kidedea kwa kufunga penati ya mwisho baada ya mlinda mlango wa Ghana Razak Braimah kukosa penati.
Shangwe na vigeregere mjini Bata, Equatorial Guinea
Shangwe na vigeregere mjini Bata, Equatorial Guinea
Mlinda mlango mkongwe wa Ivory Coast Boubacar Barry ndiye nyota wa mchezo wa leo.
Mlinda mlango nambari mbili wa Ivory Coast ndiye aliyepia ushindi timu yake
Mlinda mlango nambari mbili wa Ivory Coast ndiye aliyepia ushindi timu yake
Mwaka 1992, Ivory Coast waliifunga Ghana kwa mikwaju ya penati 11-10.
Ghana walipata penati 8 huku Ivory Coast wakishinda kwa penati 9
Ghana walipata penati 8 huku Ivory Coast wakishinda kwa penati 9
Mashindano hayo yalikuwa yanafanyika nchini Equatorial Guinea.

BOSS WA MJ RECORDS AFUNGUKA


 
Mtayarishaji mkongwe wa muziki nchini, Master J amekuwa mstari wa mbele kupaza sauti kuhusiana na kutokuwepo kwa usawa kati ya watayarishaji wa muziki na wasanii nchini.
Master J ameiambia Bongo5 kuwa kuna watayarishaji ameshaona wanakosa moyo wa kufanya kazi kutokana hali hiyo.

Tanzania maprodyuza ni maskini, eti wasanii wana hela kuliko producers hii ni industry gani,” amehoji Master J. “Kwa sababu hapa hizi sheria zilizopo hazimlindi producer ndo maana anadharaulika. Huyo huyo msanii yupo tayari akulipe laki mbili umtengenezee wimbo halafu anauchukua huo wimbo kwenda kutengeneza video kwa milioni 25 yaani wewe acha tu, hiyo ni dharau kubwa sana,” ameongeza.

Yaani mimi nikiangalia industry nacheka tu, ni matusi. Huyo huyo producer unaweza ukamlipa milioni ukishamlipa milioni asikusumbue tena kwenye revenue share. Yaani unashindwa kumthamini producer hata umlipe milioni kwa sababu ile laki mbili unayolipia ni studio time lakini haujanunua haki yangu. Mimi naona pale wewe sasa hivi huangalii hata Marco ameacha kufanya kazi unafikiria kwanini?"

Amevunjika moyo yaAni moyo wake umevunjika kabisa kwa sababu anaonyeshwa laki mbili halafu huyo huyo anayeonyesha lakini mbili anaenda South Afrika anashoot video ya dola elfu kumi na tano, bila beat huo wimbo wake utaenda wapi? Bila beat wimbo wako utapigwa r
redioni? Unajua maproducer itafika sehemu watachoka kwa sababu sasa hivi wengi wameshaanza kuona dharau, kishingo upande wanalalamika.

Mjue nyota wa muziki :Anayesema kuwa atapatana na mtu atakayekiri kosa


Msanii wa bongo Fleva Judith Wambura maarufu kama Lady Jaydee amefunguka na kuweka wazi kuwa katika maisha yake ya kawaida, maisha ya sanaa na maisha ya utafutaji amekuwa akikutana na changamoto mbalimbali.
LadyJaydee
Changamoto hizo wakati mwingine hupelekea watu kugombana au kutofautiana kutokana na mtazamo au matatizo mbalimbali na amedai wazi kuwa katika watu wote ambao aligombana nao na yeye kugundua ndiye alikuwa chanzo cha ugomvi huo wote alishawaomba msamaha na wanaendelea na maisha ya kila siku.
Lady Jaydee alisema hayo jana kupitia ukurasa wake wa Instragram wakati akijibu maswali 10 yaliyotokana na maswali kibao kutoka kwa mashabiki wake.
“Nitapatana na mtu atakae kubali kuwa alikosa, kama naamini yeye ndio alinikosea itabidi aniombe msamaha. Kama mimi ndio nilikosa nitaomba pia msamaha Otherwise hakuna miujiza Siwezi kumuomba mtu msamaha endapo naamini kabisa sijakosa .
Niliowahi kuwakosea nilishawaomba msamaha wooote.Hakuna binadamu asiye kosea ila siwezi ku surrender kiuongo au kwa uoga wa maisha.
Naamini hata nikiuza nyanya bado wapo watu wanaohitaji nyanya, na watanunua.”
Baadhi ya mashabiki waliuliza kwanini Lady Jaydee hana ushirikiano na wasanii wenzake wa kike katika muziki na yeye aliweka wazi kuwa amekuwa akishirikiana nao sana tu mpaka kufikia hatua wengine kuwatungia wimbo, Jide anadai kuwa mara nyingi ili msanii aweze kutoka au kufanya vizuri lazima kazi zake zipate promo ya kutosha katika vituo mbalimbali vya Radio lakini bahati mbaya yeye sio mwenye hizo Radio.
“Nimewahi kufanya na wasanii mbalimbali wa kike ila sijui kwanini hamjaziskia.
1. Mwasiti amewahi kunishirikiisha
2. Nimewahi kumuandikia na kushiriki kuimba kwenye wimbo wa movements za Albino na Keysha
3. Nimewahi kumwandikia na kushiriki kuimba na Nakaaya Sumari
4. Nimewahi kumwandikia wimbo Patricia Hillary
5. Nimewahi kumshirikisha RAY C kwenye wimbo wangu toka Album ya Machozi unaitwa, Nimekubali na wapo wasichana mbali mbali waliopita Machozi Band na kujifunza kuimba leo mnawafahamu, Kumbukeni tu kuwa kutoka kwa mtu itategemea na nyimbo zake kuwa promoted redioni na mimi sio mwenye hizo redio .
Msaada pekee ni kushiriki kila ntakapotakiwa kufanya hivyo”
Lady Jaydee kwa sasa anatamba na wimbo wake wa Forever ambao amemshirikisha mdogo wake anaefahamika kama Dabo na pia mwanadada huyo amepanga kufunguka mengine mengi katika kipindi chake kinacho ruka eatv.tv

Saturday, February 7, 2015

Mbasha akana kukitambua kichanga cha mkewe


Emmanuel Mbasha amekiambia kituo cha redio cha SunRise kuwa hajuo kuwa mkewe amejifungua mtoto
Emmanuel Mbasha amekiambia kipindi cha redio cha SunRise -Times FC kuwa hajuo kuwa mkewe Flora Mbasha amejifungua mtoto
Familia ya Mbasha inaendelea kutengeteza vichwa vya habari, baaada ya mchungaji maarufu nchini Gwajima kukanusha kuwa si baba wa mtoto wa Flora Mbasha, mume wa muimbaji huyo wa injili Emmanuel naye ameibuka na kudai kuwa hatambui chochote kuhusu kuzaliwa kwa mtoto huyo.
Mbasha ambaye pia ni muimbaji wa muziki huo wa injili amesema anachojua ana mtoto mmoja wa kike anaeitwa Lizy mwenye umri wa miaka kumi na hizo taarifa za Flora kajifungua anazisikia kwa watu wengine.
Mtoto aliyezaliwa na mwanamuzki wa injili Flora Mbasha
Mtoto aliyezaliwa na mwanamuzki wa injili Flora Mbasha
“Nina mtoto mmoja, nina mtoto mmoja anaitwa Lizy ana umri wa kama miaka 10 hivi! Wewe ndo unanieleza mimi kama amejifungua, kama amejifungua, ni jambo jema na la kumshukuru Mungu,” alieleza Emmanuel Mbasha
Mbasha alikiambia kipindi cha SunRice Times Fc.

Bikini Yazua Mjadala huko Instagram


Picha hii imepostiwa kupitia Account ya msanii wa Nay Wamitego ya Instagram akiwa yupo kitandani na mwanadada ambae amevalia bikini huku sehemu kubwa ya mwili wake ukiwa wazi unaonekana ila badae Nay alitoa picha hiyo.
Hali ya mwanadada huyo ameonekana akitabasamu bila kuwa na wasi wasi kitendo ambacho kinafanya tuamini kwamba labda wana shoot video, lakini sidhani kama ni sawa pia kwa maadili yetu ya Kitanzania.
Nay Wamitego
Pengine si vibaya lakini mazoea hayo kwetu Watanzania ni mageni.
Picha hii imeonekana kuchukiza mabinti wengi na kuenea kwa story tofauti kwa muda mfupi tangu aipost.

Haya hapa Maneno ya Uchungu ya Wastara Juma



Wastara Atoa Maneno ya Uchungu, Yawagusa Wengi!
Muigizaji wa filamu,Wastara Juma amewapa watu simamzi zito mtandaoni, baada ya leo kuandika maneno mazito ya uchungu akisema matatizo ya dunia yamemzidia na kubandika picha akiwa analia. Na hivyo kupelekea mashabiki wengi kumpa pole na kumtia moyo kuwa yote yana mwisho wake na Mungu ndio mpagaji wa yote.
"Hapa duniani kila mtu ana shida na matatizo lakini kwangu mimi yamezidi daaah eeeh Mungu nibadilishe basi hiyo nafasi ya mteso uliyoniweka muweke mwingine nami unipe furaha nicheke kama wengine maishani mwangu niache kulia eeeh Mungu baba jamani mimii mimiii aah".-Wastara aliandika baada ya kuweka picha hiyo hapo juu.
Hakuweka wazi nini hasa kimempata,lakini picha hii inaonekana imetoka kwenye moja ya kipande cha filamu.
Chanzo:http://www.bongomovies.com/