Holyfield amejitosa sakata la mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uruguay Alberto Suarez anayekabiliwa na shitaka la kumng'ata beki wa timu ya taifa ya Itali Giorigio mbele ya Kamati ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).
Cameroon sasa wameenda Brazil baada ya mzozo kuhusu marupurupu yao kutatuliwa.
Wachezaji hao , almaarufu 'Indomitable Lions' walikuwa wamesusia kuingia ndegeni hadi marupurupu yao yaongezwe.
Akiwemo nyota wao mshambuliaji wa
Chelsea, Samuel Eto'o, walikuwa wamegoma kuingia ndegeni hapo Jumapili
asubuhi hivyo safari ikachelewa kwa zaidi ya saa 12.
Wachezaji hao walikuwa wakilalamikia kiwango cha fedha £61,000 ambazo walikuwa wamepangiwa kupewa wakisema hazingetosha.
Haijabainika vyema ni idadi gani walichoongezewa ndio wakakubali safari.
Hata hivyo rais wa shirikisho la soka la
Cameroon Bw.Joseph Owona amesema 'baada ya kuweka kila kitu wazi ,mzozo
huo umetatuliwa na sasa hamna tatizo'.
Tatizo lililopo sasa kwa masimba hao ni kupata
mkakati madhubuti wa kukabiliana vilivyo na timu za kundi lao A ambamo
wamo miamba ya soka wenyeji Brazil, Croatia na Mexico.Source BBC.