Msanii na mmiliki wa Bendi ya Malaika Band,
Christian Bella amefunguka na kusema anamshukuru Mungu uwezo wake
kimuziki unazidi kuwa juu kila siku.
Msanii Christian Bella akifanya yake stejini
Christian
Bella ni kati ya wasanii ambao walifanya vizuri na kuweza kukonga
nyonyo za mashabiki wengi walitokea katika shoo ya Wizkid pale Leaders
Club siku ya Jumamosi ya wiki iliyopita.
Akipiga stori katika kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio,
Bella amesema shoo ile ilikuwa ngumu lakini aliipenda kwa sababu
walipata nafasi ya kutosha kuimba kwa nafasi jambo ambalo lilifanya
mashabiki waweze kusikia nyimbo nyingi zikiwa zimekamilika tofauti na
shoo nyingine ambazo huwa wanaimba nyimbo nusu nusu ili kupisha wasanii
wengine nao waweze kuimba.
"Shoo za wazi kama hizi huwa zinakuwa ngumu sana lakini nashukuru
Mungu niliweza kufanya shoo na watu walinielewa ila niliipenda shoo kwa
sababu tulikuwa tunanafasi ya kuimba nyimbo nyingi nzima bila kukata
kata,” alisema Bela na kuongeza “Unajua kwenye shoo nyingi za wazi huwa
tunaimba viitikio tu na sehemu maalumu za wimbo ili kupisha wasanii
wengine nao waweze kuimba lakini hii imekuwa tofauti, ingawa ilikuwa
ngumu kwa msanii maana ilikuwa lazima ujipange vyema kuwa na orodha ya
nyimbo nzuri ili uweze kuwapa raha mashabiki na nilifanikiwa katika
hilo" .
Christian Bella, Fid Q pamoja na Diamond walimsindikiza vyema Wizkid
katika shoo hiyo ambapo wasanii hao waliweza kufanya shoo Live kwa
kutumia bendi.
No comments:
Post a Comment