
Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Marie Stopes Tanzania (MST), Uller Muller (kulia)
akikabidhi kisanduku chenye vifaa vinavyohusika na masuala ya uzazi wa
mpango kwa Balozi mpya wa Marie Stopes ambaye pia ni msanii mkongwe wa
muziki wa kizazi kipya, Judith Wambura ‘Lady jaydee’ katika hafla ya
utiaji sahihi makubaliano hayo katika ofisi za MST, jijiji Dar es Salaam
jana.
Mwanamuziki Lady Jaydee ametuliwa na Hospitali ya Marie Stopes kuwa
balozi wa kampeni ya kuhamasisha uzazi wa mpango na kupinga mimba za
utotoni inayoitwa ‘Chagua Maisha’.
Akiongea na TBC, Lady Jay Dee amesema kuwa anaweza kufikisha ujumbe
kwa jamii kwa kuimba nyimbo ambazo zitasaidia kuwahamasisha wananchi
kuchagua jinsi ya kuishi kwa kutumia uzazi wa mpango.
No comments:
Post a Comment