Shirika la upelelezi la Marekani (FBI) linachunguza tuhuma kwamba picha za siri za watu maarufu ziliibiwa na kutumwa mtandaoni.
Mastaa hao wapatao 20, akiwemo muigizaji wa kike wa Marekani Jennifer
Lawrence, naye picha zake zilivujishwa kwenye mtandao wa Internet.
Inafahamika kuwa baadhi ya picha hizo zilipatikana katika huduma ya Apple iCloud ambayo husaidi ujumbe uliopo mtandaoni.
Apple nao imesema inachunguza kuwa kama akaunti ya iCloud ilifanyiwa udukuzi.
Bi Lawrence, ambaye ni nyota katika filamu za The Hunger Games,
ameomba kufanywa uchunguzi baada ya mdukuzi kupata picha, zenye ujumbe
wa picha, kutoka simu za mkononi za mastaa kadhaa.
Msemaji wa FBI aliiambia Associated Press kwamba “wako makini na tuhuma hizo na wanalishughulikia suala hilo”.
Naye msemaji wa Apple Nat Kerris alinukuliwa na Reuters akisema
kwenye barua pepe; “Huwa tunalinda faragha za watumiaji kwa umakini
mkubwa na tunachunguza ripoti hii.”
No comments:
Post a Comment