Mmoja kati ya watuhumiwa wawili wanaoshutumiwa kuwashikilia wanawake watatu katika mazingira ya utumwa kwa miaka 30 mjini London anatokea Tanzania, polisi Uingereza wamesema Jumamosi.
Kamanda wa polisi wa London Steve Roadhouse amesema watuhumiwa hao, ambao ni mke na mume wenye umri wa miaka 67, ni wahamiaji waliokwenda London kwenye miaka ya 1960 kutoka India na Tanzania.
Polisi wanahisi watuhumiwa hao walikutanishwa na wanawake hao watatu katika "harakati za kisiasa" zilizopelekea waanze kuishi "kijamaa" kwenye nyumba moja.
Haijulikani hali ilibadilika vipi, lakini inaelekea kwenye miaka ya 1980, kibao kilibadilika, na wanawake hao watatu wakajikuta wakigeuzwa vitwana wa timu hiyo ya mke na mume.
No comments:
Post a Comment