skills za kitaa

Tuesday, May 6, 2014

Peter wa P Square anunua gari lenye Thamani ya sh. Milioni 300


MSANII nyota  Peter Okoye wa nchini Nigeria toka katika kundi maarufu la 'P-square' ameamua kuonesha Jeuri ya kuzidi kumiliki pesa ndefu baada  ya kuonesha Gari Yake Mpyaa yenye thamani ya zaidi Milioni 300 za kitanzania.

 Hali hiyo ya ununuaji wa gari hilo la kifahari imekuja siku chache tu baada ya kumaliza matatizo yao kwenye familia na ndugu zake,matatizo  ambayo bado hayajajulikana kama yalikuwa ni kweli au ni amsha amsha za kibiashara zao za kimuziki.


kwa siku za karibuni imesemekana yeye na ndugu zake wawili  hawakuwa kwenye maelewano kwa kipindi kifupi lakini sikuchacheche zilizopita wameweza kuandika ku- tweet maneno ambayo yaliashiria wamemaliza tofauti zao.

No comments: