Ukitaka kuongea muziki wa dansi uliingiaje nchini ni muhimu kujua historia ya mji wa Tanga. Wadau wanasema mji wa Tanga ndipo muziki wa dansi ulipoingilia nchini.
Wajerumani waliusambaratisha mji wa Tanga kwa
mizinga kati mwaka 1888 na 1889. Na baada ya hapo
kuujenga upya kwa kufuata mpangilio uliosababisha
Tanga kuwa na mitaa maarufu kama barabara ya kwanza
ya pili na kuendelea.
Wajerumani walianzisha shule ya kwanza ya serikali
Tanga 1892 na hapohapo wakanzisha bendi ya shule ya
kwanza, pamoja na kuwa Wajerumani hawakutawala muda
mrefu baada ya hapo lakini Waingereza waliiendeleza
sana bendi hiyo iliyokuwa ikipiga aina mbalimbali za
muziki wa kigeni.
Dansi ilianza kwanza kama klabu ambapo watu
walialikana kuja kucheza aina mbalimbali za muziki wa
kizungu mtindo maarufu unaojulikana kama 'ballroom
dancing'.
Aina hizi za klabu zilianzia Mombasa na
kuingia nchini kupitia Tanga na kisha kuletwa Dar es
Salaam na klabu iliyokuwa maarufu Tanga ili kujulikana
kwa jina Tanga Young Comrades Club, klabu nyingine
ilianzishwa ikaitwa New Generation Club ambayo
ilianzisha matawi miji mbalimbali.
Wadau wa elimu waliupoteza muziki, kwa miaka
ya nyuma katika kila shule kulikuwa kunafundishwa
somo la muziki lakini kwa kadri siku zinavyoenda
somo hilo linaonekana kupotea.
Msanii nguli katika muziki wa dansi nchini
John Kitime anasema kuwa takriba kila shule
ya sekondari miaka ya nyuma kulikuwa na kipindi
cha muziki ambapo mwanafundi aliweza kujifunza
muziki.
"Tulukuwa na aina za muziki , tulitumia sana
muziki wa Afro na wanafunzi katika kipindi hicho
cha miaka ya nyuma aliweza kuchagua aina ya sanaa.
"Wapo wanafunzi wengine walipendelea kujifunza
muziki wa asili tu , nao walikuwa na nafasi yao,
kwa kweli kila sanaa ilifundishwa katika kipindi
cha muziki shuleni,"anasema Kitime.
"Tulikuwa tukikutana na shule zingine katika masuala
ya kupiga muziki ali iliyochochea mafanikio ya
wanamuziki wa dansi kupatikana nchini tofauti na
sasa."
Kitime ambaye ni mdau katika medani ya
muziki nchini anasema kuwa kutokana na mambo
yanavyokwenda kwa hivi sasa katika taswira ya sasa
katika muziki wa sasa ambao ni Bongoflava.
Kitime anapasua jambo kwa kusema kuwa hali ya
kutofundishwa masomo ya muziki kama yaliyokuwepo
awali ndio haswa mpasuko katika muziki.
"Bendi nyingi za dansi zilizowai kuwika wanamuziki
wengi walianzia kuwika na kuonekana vipaji vyao
wakiwa bado shuleni sehemu waliyo pata kufundishwa
masomo ya muziki.
"Kwa sasa Tanzania haijulikani inafanya muziki wa
aina gani kwani hatuna tena asili ya muziki wa
Tanzania kama ilivyo wai kuwepo, wanamuziki wengi
walipata kutia heshima katika anga za muziki miaka ya
nyuma.
Kuhusu yeye kushauri vijana wa muziki wa Bongoflava
anasema awezi kushauri kitu chochote katika muziki
huo kwa sababu yeye ajapata kuujua maka sasa
aufahamu.
"Siwezi nikashauri kituambacho mimi sikijui ,
mie siujui muziki huo na sijawai kufanya muziki
wa aina hiyo , sasa siwezi kushauri chochote,
mtu anashauri kituanacho kifahamu,"anasema Kitime.
Kitime anasema kuhusu kelele za wasanii kuibiwa
kazi zao wasanii nyota huyo mkongwe katika anga za
muziki wa dansi ana tiririka kwa kusema kuwa.
"Wadau wa muziki wanakuwa wanailaumu serikali ,
kuwa wanaibiwa kazi zao za muziki lakini wao
wanawajua wezi wao , kimusingi anatakiwa alaumiwe
anayemjua mwizi .
"Na si serikali kwani vyombo vya sheria vipo
mtu anatakiwa akamate mwizi na kumpeleka
katika vyombo husika na kitendo cha kulalamika tu
mdomoni na kusema serikali haiwajali, na wakati wao
wanamjua mwizi wao aitoshi kumkataza mwizi asiibe."
Kitime anapasua tena jibu kwa kusema kuwa yeye
ametoka katika familia ya muziki kwani mama na baba
yake ni wazazi ambao waliopata kufahamika katika
tasnia ya muziki hivyo hali hiyo ilimfanya yeye
kuchochea nyota yake kunga'ra katika tasnia ya muziki
wake.
Pia John Kitime ni mtu ambaye hachoki kuhifadhi na
kusambaza historia ya muziki nchini Tanzania kuanzia
ule tuliouita 'Muziki wa Dansi' .
Kitime anafanya hivyo kwa kutambua kwamba endapo
juhudi binafsi hazitofanywa,basi kizazi cha Tanzania
cha miaka kumi ijayo,hakitojua wapi tulitoka katika
medani za muziki.
Wataanzia tulipo na pengine kuishia tulipo.Wadau
kadhaa wameisha wai kumuomba Kitime asisahau
kuandika kitabu ili kuhifadhi vizuri zaidi historia
muhimu.Kwani kitime hadi sasa ni mdau wa ulimwengu
wa sasa anaye elimisha jamii kupitia mitandao
ya kijamii anamiliki Blog tano za kijamii.Inatoka gazeti la Majira.
No comments:
Post a Comment