skills za kitaa

Sunday, August 25, 2013

Soma stori hii



Dee Sala ni msanii wa Hip-hop hapa TZ, lakini this time ameamua kubadilika,
amegeukia upande wa pili wa bongo flava. Badala ya kuchana (rapping) sasa
ameamua kuimba. Msanii huyu ametua na ngoma mpya ya RnB iliyotengenezwa
 na Mr T Touchez kutoka Seductive Records.
Dee Sala

Wimbo huu unaitwa Nakupendaga, umekuja baada ya wimbo wa Mtoto wa
 Zarumba ambao Dee Sala alirap mwanzo mwisho. Mwenyewe amekiri kwamba
 hajaacha kufanya Hip-hop kwani ndio maisha yake! Wimbo ni mzuri sana,
umetengenezwa kwa ustadi mkubwa.
Dee Sala ni msanii wa Hip-hop hapa TZ, lakini this time ameamua kubadilika, amegeukia upande wa pili wa bongo flava. Badala ya kuchana (rapping) sasa ameamua kuimba. Msanii huyu amekuja na ngoma mpya ya RnB iliyotengenezwa na Mr T Touchez kutoka Seductive Records.
Dee Sala

Wimbo huu unaitwa Nakupendaga, umekuja baada ya wimbo wa Mtoto wa Zarumba ambao Dee Sala alirap mwanzo mwisho. Mwenyewe amekiri kwamba hajaacha kufanya Hip-hop kwani ndio maisha yake! Wimbo ni mzuri sana, umetengenezwa kwa ustadi mkubwa. - See more at: http://www.keezywear.com/#sthash.jMusVq19.dpuf
Dee Sala ni msanii wa Hip-hop hapa TZ, lakini this time ameamua kubadilika, amegeukia upande wa pili wa bongo flava. Badala ya kuchana (rapping) sasa ameamua kuimba. Msanii huyu amekuja na ngoma mpya ya RnB iliyotengenezwa na Mr T Touchez kutoka Seductive Records.
Dee Sala

Wimbo huu unaitwa Nakupendaga, umekuja baada ya wimbo wa Mtoto wa Zarumba ambao Dee Sala alirap mwanzo mwisho. Mwenyewe amekiri kwamba hajaacha kufanya Hip-hop kwani ndio maisha yake! Wimbo ni mzuri sana, umetengenezwa kwa ustadi mkubwa. - See more at: http://www.keezywear.com/#sthash.jMusVq19.dpuf
Dee Sala ni msanii wa Hip-hop hapa TZ, lakini this time ameamua kubadilika, amegeukia upande wa pili wa bongo flava. Badala ya kuchana (rapping) sasa ameamua kuimba. Msanii huyu amekuja na ngoma mpya ya RnB iliyotengenezwa na Mr T Touchez kutoka Seductive Records.
Dee Sala

Wimbo huu unaitwa Nakupendaga, umekuja baada ya wimbo wa Mtoto wa Zarumba ambao Dee Sala alirap mwanzo mwisho. Mwenyewe amekiri kwamba hajaacha kufanya Hip-hop kwani ndio maisha yake! Wimbo ni mzuri sana, umetengenezwa kwa ustadi mkubwa. - See more at: http://www.keezywear.com/#sthash.jMusVq19.dpuf

LEWANDOSKI: KWANINI NILIKATAA KUJIUNGA NA MAN U, MADRID NA CHELSEA.



shakle 6b03c 
Mshambuliaji wa Borussia Dortmund Robert Lewandowski amefunguka na kusema kwamba amekataa kujiunga na vilabu vya Manchester United, Chelsea na Real Madrid ili aendelee kucheza kwenye Bundesliga.

Matapeli waigusa ikulu



IKULU a4b39MTANDAO hatari wa matapeli unaotumia mbinu mbalimbali, ikiwemo za kujipachika vyeo vya maofisa usalama wa Taifa, sasa umefanikiwa kupenya na kuanza kutumia viunga vya Ikulu iliyopo Magogoni, Jijini Dar es Salaam, kufanikisha hujuma zao.
Taarifa zimethibitisha pasipo shaka kwamba Ikulu ya Jijini Dar es Salaam sasa inataka kugeuzwa kuwa kichaka na matapeli hao, ambao pia wamejivika undugu wa kifamilia na viongozi wakubwa nchini.
Mtandao huo, ambao unaaminika kuumiza watu mbalimbali, ukiwalenga zaidi akina mama na wanafunzi wa vyuo vikuu nchini, anayetumikia kufanikisha utapeli huo kupitia viunga vya Ikulu, ni mvulana anayejiita Baraka Tibaijuka.

Historia March Miaka 50 tangu kutoa hutuba mwanaharakati Martin Luther King Jr."I Have a Dream" speech Washington DC


Maelfu ya wananchi kutoka sehemu mbalimbali nchini  wamejitokeza kwa wingi jijini Washington DC Siku ya Jumamosi  Aug 24, katika maandamano ya kuunga mkono kumbukumbu ya  historia  March Miaka 50 tangu kutoa hutuba mwanaharakati Martin Luther King Jr."I Have a Dream" speech Siku ya Aug. 28, 1963
Picha ya kumbukumbu ya  historia  ya   mwanaharakati Martin Luther King Jr. alipokua akitoa hotuba ya "I Have a Dream" speech  Aug. 28, 1963 /photo google.
Maandamano hayo makubwa yaliofanyika National Mall yaliambatana na hotuba mbalimbali za wanaharakati, na viongozi wakupigania haki mbalimbali za kiraia nchini Marekani,  kulisomwa hutuba mbalimbali na mwanasheria mkuu wa Serikali Eric Holder, Ufunuo Al Sharpton; Rep John Lewis, D-Ga;. Nyumba Minority Kiongozi Nancy Pelosi, D-Calif;. House Minority Whip Steny Hoyer, D-Md; Myrlie Evers-Williams, mjane wa waliouawa mwanaharakati wa haki za kiraia Evers MEDGAR; Newark, NJ, Meya na New Jersey Kidemokrasia Seneti mgombea Cory Booker; Mama wa Trayvon Martin, na viongozi wa makundi ya kiraia-haki za binadamu.
Kumbukumbu ya Hutuba ya Dream" speech ilitolewa mwenzi wa  Aug. 28, 1963 ambayo ilihudhuriwa na umati mkubwa wa wananchi National Mall.





 Wanaharakati mbalimbali waliokusanyika Lincoln Memorial Washington DC wakitoa hotuba Historia March Miaka 50 tangu kutoa hutuba mwanaharakati Martin Luther King Jr."I Have a Dream" speech  Washington Wananchi mbalimbali waliojitokeza Lincoln Memorial  katika maandamano yaliofanyika Washington DC National Mall Siku ya Jumamosi Aug 24, 2013 Wananchi wengi waliojitokeza katika maandamano yaliofanyika Washington DC National Mall Siku ya Jumamosi Aug 24, 2013 Wanachi waliobeba mabango yenye ujumbe unaohuso haki za binaadamu wakitembea National Mall  kuelekea  Lincoln Memorial Washington DC
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye maandamo wakiwa wameshikilia bango lenye ujumbe wa Trayvon Martin kijana alieuwawa kwa kupigwa risasi na mtu mwepe.




Saturday, August 24, 2013

TIKETI ZA ELEKTRONIKI KUANZA MZUNGUKO WA NNE

simba 5f6a3
Tiketi za elektroniki zitaanza kutumika katika mzunguko wa nne wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) utakaoanza Septemba 18 mwaka huu. Tayari benki ya CRDB ambayo ndiyo ilishinda tenda hiyo imeshakamilisha ufungaji wa vifaa kwa ajili ya matumizi ya tiketi hizo katika viwanja vyote. (HM)

Hivi sasa Serikali ambayo ndiyo inamiliki Uwanja wa Taifa, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) pamoja na CRDB zinashughulikia mfumo wa tiketi hizo kwenye uwanja huo ambao ndiyo ulikuwa haujakamilika kwa matumizi katika upande huo.
Mfumo (system) iliyoko kwenye uwanja huo inapishana na ule utakaotumiwa na CRDB, hivyo pande husika zinashughulikia suala hilo ili mifumo hiyo iweze kuingilia.
Pia mashine za kuchapia (printer) kwa ajili ya tiketi ambazo CRDB wameziagiza kutoka nje ya nchi zinatarajiwa kuwasili mwishoni mwa mwezi huu.
Hivi sasa CRDB inashughulikia ufungaji wa vifaa vya matumizi ya tiketi za elektroniki iwemo turnstiles kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi ambao mwanzoni hakuwemo kwenye mpango huo kutokana na Mkoa wa Tabora kutokuwa na timu ya Ligi Kuu.
RATIBA YA LIGI WIKIENDI HII
Michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu wa 2013/2014 inaanza kutimua vumbi kesho (Agosti 24 mwaka huu) katika viwanja saba tofauti huku mabingwa watetezi Yanga wakianza kutetea ubingwa wao kwa kuikaribisha Ashanti United kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Uwanja wa Manungu ulioko Turiani mkoani Morogoro utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Azam ya Dar es Salaam na wenyeji Mtibwa Sugar. Oljoro JKT itaikaribisha Coastal Union kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha.
Mgambo Shooting itaoneshana kazi na JKT Ruvu ambayo hivi sasa iko chini ya Kocha Mbwana Makata. Mechi hiyo itachezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga wakati Rhino Rangers itakwaruzana na Simba katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
Mbeya City iliyopanda VPL msimu huu itapimana ubavu na Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya huku Ruvu Shooting ikiialika Mabatini, Mlandizi timu ya Tanzania Prisons kutoka Mbeya.
Mzunguko wa pili wa ligi hiyo utachezwa Agosti 28 mwaka huu. Baada ya hapo ligi itasimama kupitisha mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kati ya Gambia na Tanzania (Taifa Stars) itakayochezwa Septemba 7 mwaka huu jijini Banjul. VPL itaingia mzunguko wa tatu Septemba 14 mwaka huu. Chanzo: tff

MAN UNITED YAKARIBIA KUWANASA BAINES, FELLAINI



moyes 58406
 Kocha wa Man United, David Moyes (HM)
Read more...

Woga watanda kwa vijana weusi Marekani;



marekani_51d0a.jpg
Mama wa Trayvon Martin, kijana Mmarekani mweusi aliyeuliwa Florida mwaka jana wakati akielekea nyumbani, anasema kufutwa kwa kesi ya mwanamgambo wa kulinda mitaa aliyemuuwa kumewafanya vijana wengi weusi wa Marekani kuwa waoga.