skills za kitaa

Sunday, June 23, 2013

Miaka 13 ya Kikosi cha Mizinga




 Chid Benz akikonga nyoyo za mashabiki wake wakati wa shoo ya Kikosi cha Mizinga kutimiza miaka 13 iliyofanyika katika ukumbi wa New Msasani jijini Dar es salaam. (Picha zote na Habari Mseto Blog).
 Chid Benz
 Fukuda akichana mistari
 Katibu wa CUF, Julius Mtatiro ambaye alikuwa mgeni rasmi  akizungumza wakati wa shoo maalumkundi la muziki wa Hip Hop la Kikosi cha Mizinga kutimiza miaka 13.
Baadhi ya watu waliotoa mchango mkuwa kwa wasanii wa Kikosi cha Mizinga walipewa vyeti, hapa mwandishi Joseph Zablon akionesha cheti chake baada ya kukabidhiwa ba mgeni rasmi. 
 Mwakilishi wa Clouds Radio akipokea cheti.
   
 Kala Pina 'Nabii Koko' akitumbuiza
 

 Afande Sele akipagawisha  mashabiki.

 

KANYE WEST NA KIM KARDASHIAN MTOTO WAo ANAITWA NORTH WEST




Rapper Kanye West na Kim Kardashian wamekuwa wasiri kuhusu mtoto wao kuanzia jinsia yake kabla hajazaliwa lakini hata baada ya kuzaliwa wamekuwa na kigugumizi cha kuliweka wazi jina la mtoto wao wa kike waliyempata June 15 mwaka huu.

Japokuwa wameficha jina la mtoto wao, cheti cha kuzaliwa cha mtoto huyo kimeongea…chanzo cha kuaminika kimeuambia mtandao wa TMZ kuwa cheti hicho kimeonesha jina la kichanga wao kuwa ni ‘North West’.

Well, wameamua kutumia dira zaidi kupata jina la mtoto au labda ni kwa sababu baba nae anajina la dira ‘West’ ambalo linatoka kwenye familia yake,marehemu mama yake aliitwa Donda West.Tetesi za awali ziliwahi kulitaja jina hili, lakini baadae ikasemekana wanaweza kutumia utaratibu wa familia ya Kardashians ambayo majina yao lazima yaanze na herufi ‘K’.

Kwa mujibu wa US Weekly, mtoto huyo tayari ameshapata jina la ki-digital yaani a.k.a na anaitwa ‘Nori’ kama ufupisho wa jina lake. Kwa upande mwingine, imesemekana kuwa Kanye West hayuko tayari kufanya biashara kwa kuuza picha za mtoto wake kama alivyowahi kufanya Angelina Jolie na Brad Pitt mwaka 2008 walipouza picha za mtoto wao kwa kiasi cha dola million 14.
Lakini baba North West hapendi kupigwapigwa picha na labda asiingependa mwanae pia aingie kwenye lens za paparazzi, chanzo kimeoja kimesema inawezekana Kim Kardashian akaamua kuzitoa bure picha za mtoto wao kwa kuwa ana hulka ya kupiga picha.
Inasemekana Weezy (36) mwenye mzuka wa ajabu wa kuandika na kutema mistari anaweza kuachia nyimbo nne maalum kwa mwanae Nori..kama alivyofanya swaiba wake Jay-Z alipoachia Glory kwa ajili ya Blue Ivy.

Sunday, June 9, 2013

Ofisini kwa Jimmy Master


Niliye simama ni mmiliki wa blog hii niki nimebisha hodi  kwenye ofisi za  msanii maarufu wa  filamu nchini Jimmy Master maeneo ya Magomeni Dar es Salaam.

Jimmy Maeter

Thursday, June 6, 2013

Ni Leo Leaders Jana


Ilikuwa ni mapema kabla ya waombolezaji kumiminika kwa wingi viwanja vya Leaders Club.
 Kuhusu inshu ya usalama eeee ilikuwa ni chokoza  hapa uone siku yako itavyomalizika vibaya.
Hapa kuna hali fulani hivi , utulivu ulitaka kushindikana kutokana na kutangazwa neno lililo ashilia kuanza kuaga mwli wa marehemu Ngweir. Siunaona harakati za jamaa wakirudishwa na  mbwa .

Cheki mikoko ya maana ya mastaa hawa




 Msanii wa muziki wa Bongoflava Shetta akiwa ndani ya mkoko wake.


Mwanandinga wa Klabu ya Azam FC Uhuru Seleman akisukuma mkoko wake.

Hapa ni viwanja vya Leaders Club Jumapili






Kwa siku za Jumapili jioni bendi ya Twanga Pepeta uporomosha burudani yake hapa.