skills za kitaa

Thursday, June 6, 2013

Cheki mikoko ya maana ya mastaa hawa




 Msanii wa muziki wa Bongoflava Shetta akiwa ndani ya mkoko wake.


Mwanandinga wa Klabu ya Azam FC Uhuru Seleman akisukuma mkoko wake.

Hapa ni viwanja vya Leaders Club Jumapili






Kwa siku za Jumapili jioni bendi ya Twanga Pepeta uporomosha burudani yake hapa.

Tuesday, June 4, 2013

Pata Filamu hii ya Mogana madukani


Inafanya poa katika soko la filamu .

MBILI ZA PILIPILI ZAWANIA TUZO!


FILAMU mbili za Lost na Crush zilizotengenezwa na Kampuni ya Pilipili Entertainment zimeingia 
katia kinyang'anyiro  cha kuwania tuzo za tamasha la filamu la nchi za majahazi mwaka huu (Ziff 2013).
Filamu hizo ni miongoni mwa filamu nyingi za kitanzania zilizochaguliwa kuwania tuzo katika tamasha hilo,
Filamu ya Lost iedairektiwa na  wakati filamu ya Crush imedairektiwa na Issa Wambura.
Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 29 mwezi wa sita  hadi tarehe 7 mwezi wa saba mwaka huu huko Zanzibar.
 Baadhi ya wasanii walioshiriki ni Ahmed Ulotu 'Mzee Chilo' ,Yusuf Mlela,Baby Madaha , Mama Mpangala  pampja na Muhogo Mchungu. 
Katka filamu ya Crush nyota waliocheza filamu hiyo ni Remmy Maywill, Sayuni Mero , Mbaraka Matitu
pampja na Mzee Chilo.www.pilipilimoviehouse.blogspot.com

Cheki Uwoya anavyofunguka Kwenye mtandao

"Maisha yana mambo mengi na  kila mmoja anajaribu kufanya kile ambacho anaweza kukifanya na kwa uwezo wa Mungu akafanikiwa kukikamilisha na hatimaye kufikia malengo yake  aliyonayo katika nafsi yake.
Ninacho amini mimi ni kuwa  hakuna mtu ambaye amekuja  duniani kwa ajili ya matatizo  na  machungu tu hata kama  unapitia matatizo vipi ziko tu siku za neema  ambazo  mwenyezi mungu atazileta kwako na wewe kufurahia  maisha yako hapa  ulimwenguni
 
 
Binafsi Naishi Mbezi Beach na  haya  ndiyo maisha  niliyonayo  sasa  namshukuru mungu  mimi na familia yangu  pamoja na mwanagu  Krish tunaishi katika  mazingira ya kawaida yanayotuweka  katika furaha  kila  siku".
Moja kati ya vitu ambavyo napenda na  namshukuru mungu kuvipata ni magari, Toyota Kluger ni moja  kati ya  kadhaa ambayo yapo kwenye parking yangu hapa nyumbani.



 Pozi la utulivu Irene Uwoya duu.

Jeep ni aina  nyingine ya ride ambayo sometime  nafanya  mtoko nikiwa sambamba na marafiki zangu ambao tumekuwa pamoja  tangu na tangu katika  kutafuta  maisha  na  kujiweka  katika  mazingira  tofauti kila siku.
 
 Duuu , eeeeee huyu ni Uwopya wa ukweli . Aaaaaa.

Msome Recho!

MSANII anaye fanya tasnia ya filamu
nchini Recho Haule amefunguka kuwa amekuwa akifanya mazoezi kwa sasa ili
kuimarisha mwili na si kwamba anapunguza uzito ili aolewe kama baadhi ya watu wanavyodai.

Nyota huyo mefunguka hivyo baada
ya kuibuka tetesi zilizotufikia katika
gazeti hili kutoka kwa baadhi ya wasanii wa tasnia hiyo ya filamu.


"Kwa sasa nafanya mazoezi kwaajili
ya kutunza hali ya afya yangu,nimekuwa
nikifanya mazoezi  ilikuutunza
mwili wangu uwe katika hali ya afya
njema,"alisema Recho .

Recho ambaye ni mnene kiasili ,yupo mbioni kuja na ujio mpya wa filamu iitwayo Vanessa in Dillema akiwa amewashirikisha baadhi ya wasanii wakongwe kwenye tasnia ya filamu ikiwemo Haji adam'Baba Haji',), Jennifer Kyaka 'odama' .




Mwli wa Albert Mangweha 'Ngwair' watua Dar Leo Mchana

MWILI wa nguli wa muziki wa hip hop nchini Albert Mangweha 'Ngwair' uliwasili jana kwenye uwanja 
 wa 

ndege wa Mwalimu Julius .K. Nyerere ukitokea Afrika ya Kusini alipopatwa na mauti.






Maelfu ya watu na wadau wa muziki nchini walionyesha simanzi kubwa na wengi wao kububujikwa na machozi baada tu ya kuwasili kwa mwili huo kiwanjani hapo.
Na mara baada ya kutua kwa mwili huo safari ya kuelekea katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dr es Salaam ilianza.
Wadau washangaa !
Kuona hakuna bongo movie hata mmoja aliyekuwa mstari wa mbele kama kawaida  kwenye misiba mingine
 katika uwanja huo hakuonekana ata msanii mmoja wakati marehemu alikuwa ni mtu wa watu na ukizingatia yeye ni msanii mwenzao .





 Wadau


ni T.I.D


Wadau wa habari wakiwajibika

Moja ya heka heka barabarani mwili ukiwa unaelekea Hospitali ya Taifa .